Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: vyanzo makini kutoka mji wa Musol vyatangaza kunyongwa kwa idadi kadhaa ya wanakikundi cha kigaidi cha Daesh kwa amri ya viongozi wa kikundi hicho, chanzo hicho kimebainisha njia mpya ya kuwanyonga wanachama wake wanaotaka kutoroka katika kikundi hicho, ambapo huwatia katika gari kubwa na kufunga milango ya gari hilo na kufungua gesi ndani ya gari hilo, kitu ambacho kuwafanya watu waliopo katika gari kufa kutokana na kuvuta hewa ya gesi.
Aidha kikundi cha kigaidi cha Daesh kinabuni njia za kutisha za kuwanyonga wanachama wake wanaojaribu kukimbia kutoka katika kikundi hicho, wakiwa na lengo la kuwatishia wengine na kuingiza hofu katika nyonyo zao wasikimbie kutoka katika kikundi hicho, pia kutia hofu kwa wananchi wasiokuwa wanajeshi wanaoishi katika maeneo yalioko chini ya kikundi hicho cha kigaidi wasitoke katika sehemu hizo ili kuwa ngao yao dhidi ya majeshi ya Iraq.
Inasemekana kuwa katika mwendelezo wa majeshi ya Iraq ya kuyakomboa maeneo yanayokaliwa na kikundi hicho cha kigaidi, ambapo wanajeshi wa Iraq katika sehemu ya Halidiya nchini humo wamegundua kaburi la watu wengi ambalo walikuta miili 200 katika kaburi hilo ambao wote ni katika magaidi wa kikundi cha Daesh.
Ama mpaka sasa miili ya magaidi hao haijafahamika kuwa ni miili ya magaidi ambao waliuliwa na wapiganaji wa Iraq au wameuliwa na wenyewe Daesh.
Lamuhimu kukumbusha ni kwamba kikundi cha kigaidi Daesh nchini Iraq na Syria kinafanya kila njia ili kuhifadhi maeneo waliokuwa wameyateka katika mataifa hayo, ambapo huwafanyia vitendo vibaya hata wanachama wenzao katika vikundi hivyo vya kigaidi, ambapo kikundi hicho cha kigaidi huwapa adhabu kali wananchi wa Iraq au Syria wanaotaka kuondoka katika maeneo ya magaidi hao, ama wale ambao wanakuwa katika viwanja vya mapambano wanapokimbia katika sehemu za mapambano kutokana na vita kuwa kali, hunyongwa kinyongo kibaya sana, huku kila siku wakibuni njia nzito zaidi ya kuwanyonga wanachama wao.
mwisho wa Habari/290